• Breaking News

  Kauli ya Halima Mdee Baada ya Askofu Gwajima Kumtaka Amuombe Radhi Spika wa Bunge

  Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dr. Josephat Gwajima jana  alijitokeza hadharani mbele ya waumini wa kanisa lake na kumtaka Halima Mdee Mbunge wa CHADEMA kumuomba radhi Spika wa Bunge Job Ndugai kwa maelezo kuwa alimtukana. Gwajima alisema, kama hatafanya hivyo, basi ataitumia Jumapili Ijayo 'kumchapa' Hadharani
   Kutokana na madai hayo, Halima Mdee amejitokeza hadharani na kumjibu Gwajima

  "Namuheshimu sana Mch. Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.

  "Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO."

  No comments

  Post Top Ad