• Breaking News

  Kamanda Sirro atoa tahadhari kwa wauza CD zenya Maudhui ya Kigaidi

  Katika kuhakikisha Jiji la Dar es salaam linakuwa katika hali ya usalama kwa wananchi na mali zao, Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amewatahadharisha wafanyabiashara wa CD ambazo zina viashiria vya ugaidi kuacha mara moja biashara hiyo vinginevyo hatua kali zitachuliwa dhidi yao.

  Amesema hayo Jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kama wasipotii amri hiyo ya kuacha kuuza CD hizo zenye viashiria vya ugaidi ndani yake basi Jeshi la Polisi litaanzisha msako mkali dhidi yao na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

  “Hizi CD zina viashiria ambavyo vinahamasisha watu kufanya uhalifu kama ujambazi na masuala ya ugaidi, natoa angalizo kwa wafanyabiashara hao kuziteketeza, hii ni kwa ajili tu ya kuliweka Jiji letu katika hali ya usalama zaidi,”amesema Sirro.

  Aidha, katika hatua nyingine, Sirro amewataka wafanyabishara wote wa CD wanaotandaza kando kando ya barabara kuacha mara moja kwani siyo sehemu sahihi na salama ya kufanyia biashara hiyo.

  Hata hivyo, amesema kuwa hatua mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa za kuhakikisha Jiji linakuwa salama na shwari, pia ametoa wito kwa wazazi, walezi, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kufuatilia nyendo za watoto wao ili wajue wanajishughulisha na nini.

  No comments

  Post Top Ad