• Breaking News

  TBS yatengeneza viwango 300 vya ubora

  Shirika la viwango nchini TBS wametengeneza jumla ya viwango 300 kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017 vitakavyoanza kutumika kupima ubora wa bidhaa katika sekta mbalimbali za uzalishaji ili kukuza Viwanda hapa nchini 
   
  Kaimu mkurugenzi wa TBS, Profesa EGIDI MABOFU 
   
  Shirika la  viwango nchini TBS wametengeneza jumla ya viwango 300 kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017 vitakavyoanza kutumika kupima ubora wa bidhaa  katika sekta mbalimbali za uzalishaji ili kukuza Viwanda hapa nchini

  Kaimu mkurugenzi wa TBS Profesa EGIDI MABOFU  amesema kati  viwango vilivyotengenezwa  jumla ya viwango 75 zimeshathibitishwa  na waziri wa biashara  viwanda, na uwekezaji na  vimeshaanza kutumika.

  Kuhusu kuwepo kwa bidhaa hafifu sokoni MABOFU amesema TBS imeendelea kuimarisha ukaguzi  wa bidhaa zinazotoka nje ili kuhakikisha zinaingia bidhaa zenye viwango bora na  ambazo hazitaua Soko la  Viwanda vya ndani.

  No comments

  Post Top Ad