• Breaking News

  Wananchi wajenga kituo cha polisi ili kuzuia uhalifu

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA ,AUGUSTIN OLLOMI 
   
  Wananchi katika kata  NYANZA wilayani BIHARAMULO Mkoani KAGERA, wameamua kujenga kituo cha Polisi  katika kata hiyo ili kusaidia kupunguza matukio ya uhalifu yanayotokea mara kwa mara katika kata hiyo.
  Wakizungumzia hatua hiyo, baadhi ya wananchi wameiomba serikali kusaidia kukamilisha ujenzi wa kituo hicho ili kurejesha hali ya utulivu katika kata hiyo ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakihama makazi yao kwa hofu ya matukio ya uhalifu katika kata hiyo.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA ,AUGUSTIN OLLOMI ambaye ameweka jiwe la msingi la kituo hicho cha Polisi ,amewataka wananchi hao kuungana dhidi ya uhalifu unaondelea katika kata hiyo

  No comments

  Post Top Ad