• Breaking News

  UNAIJUA SABABU YA KUPENDWA?

   

  Mapenzi ni kitu kizuri sana kama upo kwenye mahusiano sahihi na mapenzi ni kitu kibaya sana kama utakuwa kwenye mahusiano yasiyo sahihi. Umewahi kujiuliza ni kwa nini uliyenaye anakupenda sana na umewahi kupata majibu ya hayo maswali!!??black-happy-couple1-960x1200

  Kama umewahi kujiuliza na kupata majibu basi ni vizuri sana kwa upande wako na kama umewahi kumuuliza hata yeye na akakupa majibu pia ni vizuri ingawa huwa inakuwa vigumu sana mtu kukupa sababu zote kwa nini anakupenda.

  Ukiachilia mbali sababu zinginezo BINAFSI za mtu kukupenda lakini pia hizi zifuatazo ni baadhi ya sababu za kawaida tu ambazo mtu anayekupenda huwa anazo.

  1. UNAMJALI

  Hakuna kitu kizuri kama kujaliwa na unayempenda na ndio kitu muhimu sana kwenye mapenzi. Ukionyesha kujali kwenye mapenzi basi hata vitu vingine vingi huenda kwenye mstari ulio salama na hufanya mapenzi yenu kuwa nyoofu siku hadi siku.black-couple-wedding1

  2. UNAMSAIDIA

  Hiki pia ni kitu bora sana kwenye mapenzi hasa kwa kutambua kuwa mojawapo ya njia nzuri za kudumisha mapenzi ni pamoja na kusaidiana pale linapotokea tatizo lolote lile kwa mmojawapo kati yenu. Jitolee kwa kila khali kwa mpenzi wako pale anapopata shida/tatizo lolote.

  3. UNAMRIDHISHA

  Ni kitu safi sana kuwepo kwenye mahusiano ambayo kila mtu anaridhika na mwenzake. Iwe ni kwenye mambo ya kawaida au hata yale mambo ya ndani. Ukiridhika na huyo uliyenaye na ukaridhika kwa kila anachokupa basi mapenzi huenda murua kabisa.black-couple-123q4. UNAMTETEA

  Unapoonyesha kuwa upande wa mwenzi wako kwenye kila tatizo au challenge yoyote inayotokea basi huwa ni njia nzuri sana nay a msingi kudumisha mapenzi yenu. Kuna mengi yanatokea kila siku kwenu ila jitahidi kila mara kumtetea kwa lolote mbele yake isipokuwa tu labda liwe kweli amekosea na hapo mrekebishe katika hali ya kimapenzi zaidi bila kumkwaza.

  5. MVUMILIVU/HUNA TAMAA

  Hii ni kitu njema sana nay a busara sana kwenye mapenzi na hupendwa hasa na sie wanaume pale linapokuja suala la mahusiano ambapo huwa tunapenda sana wanawake wasio na tamaa na ni wavumilivu kwa lolote ndani ya mapenzi. Hatupendi wasichana wanaoshoboka kwa vitu vidogo na vya muda na kuishia kuharibu mapenzi.black-happy-couple

  6. UNAMPA CHANGAMOTO

  Unapokuwa kwenye mahusiano haina maana basi kila anachofanya mpenzi wako ni sahihi hata kama unaona anakosea. Kama unaona hayupo kwenye njia sahihi basi mpe ushauri/changamoto ili aweze kubadilika na sio kila kitu kuwa mtu wa kumuitikia ‘’NDIO’’ tu kitu ambacho hakijengi bali kinabomoa.

  No comments

  Post Top Ad