• Breaking News

  TRUMP akataa kujibu iwapo atakubali au atakataa matokeo ya uchaguzi


  Mdahalo wa mwisho wa wagombea urais umefanyika nchini MAREKANI kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Novemba nane mwaka huu
  Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha REPUBLICAN DONALD TRUMP
   
  Mgombea wa REPUBLICAN DONALD TRUMP na Mgombea wa DEMOCRATIC HILLARY CLINTON walihojiwa kwa saa moja na nusu kuhusu masuala mbalimbali.
  Miongoni mwa masuala yaliyoulizwa katika mdahalo huo ni iwapo matokeo yatatangazwa je wagombea hao wapo tayari kuyapokea ambapo TRUMP alishindwa kujibu swali hilo.
  Mara kadhaa TRUMP amenukuliwa akishutumu kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa haki kwakuwa anataarifa kuwa kura zitaibiwa.

  No comments

  Post Top Ad