• Breaking News

  Rose Ndauka Aswekwa Lupango


  Staa wa Bongo Movie Rose Donatus Ndauka anadaiwa kuswekwa lupango kwa takriban saa nne kabla ya kuchomolewa kwa dhamana.

  Sosi wetu ambaye ni mtu wa karibu wa Rose alinyetisha kuwa, staa huyo alikuwa kwenye misele na gari lake maeneo ya Kawe jijini Dar ambapo alitanua barabarani hivyo akakamatwa kisha kukaibuka tafrani iliyosababisha kufikishwa kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe alikosota kwa muda huo kabla ya kuachiwa.

  Baada ya Wikienda kunyetishiwa habari hiyo, lilimtafuta Rose ambaye alifunguka kwa kifupi:
  “Duh! Hii ishu mmeipata? Kweli ninyi siyo watu wa mchezomchezo, baada ya kuandika kuhusu Lebo ya Ndauka mnataka umbeya tu, sasa hivi nna lebo imeanza na msanii Casso aliyeimba Wimbo wa Kitonga.”

  Rose alisema kukaa kwake lupango amejifunza kwani saa nne aliziona kama miezi na kuwakumbusha watu kuheshimu sheria za usalama barabarani

  No comments

  Post Top Ad