• Breaking News

  PICHA:Hans Van Pluijm Alivyotua Mazoezini Kuagana na Wachezaji wa Yanga


  Baada ya kuamua kujiuzulu nafasi ya ukocha mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm alienda kwenye mazoezi ya klabu hiyo kwa ajili ya kuagana na wachezaji wake pamoja na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi waliosalia kwenye klabu hiyo.

  Van Pluijm aliamua kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kupata taarifa kwamba, uongozi wa Yanga umemleta kocha kutoka Zambia George Lwandamina ili kuchukua nafasi yake.

  Kwa sasa, timu itakuwa chini ya kocha Juma Mwambusi ambaye alikuwa msaidi wa Hans van Pluijm mpaka hapo klabu itakapomtangaza kocha mkuu

  No comments

  Post Top Ad