• Breaking News

  Mfalme MOHAMMED VI wa MOROCCO aanza ziara yake nchini   
   
   Mfalme MOHAMMED wa SITA wa MOROCCO amewasili nchini kwa ziara ya kiserikali yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya MOROCCO na TANZANIA
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere
  Mara baada ya ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa JULIUS NYERERE jijini DSM  Mfalme MOHAMED wa SITA  alipokelewa na mwenyeji wake Rais DKT JOHN MAGUFULI  ukaimbwa wimbo wa taifa na kupigiwa mizinga 21 .
  Katika ziara yake hapa nchini  mfalme  huyo pamoja na mambo mengine, atasaini mikataba 11 ya ushirikiano katika sekta za kilimo, gesi mafuta reli ya LIGANGA na MCHUCHUMA na sekta ya utalii.
  Pia atatembelea ZANZIBAR na kukutana na Rais ALI MOHAMED SHEIN na pia atatembelea Mamlaka ya Hifadhi ya NGORONGORO na kujionea vivutio vilivyopo nchini.

  No comments

  Post Top Ad