• Breaking News

  MAMELODI SUNDOWNS watwaa taji la klabu bingwa AFRIKA  MAMELODI SUNDOWNS ya AFRIKA KUSINI jana usiku ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya ligi ya mabingwa barani AFRIKA pamoja na kufungwa bao moja kwa bila na ZAMALEK ya MISRI
   
  MAMELODI SUNDOWNS ya AFRIKA KUSINI
   
  Timu hiyo ya AFRIKA KUSINI imetwa taji hilo baada ya kupata ushindi wa jumla wa bao tatu kwa moja ambapo ilishinda mchezo wa awali kwa bao tatu kwa bila na jana wakafanikiwa kulinda ushindi wao walioupata nyumbani na kufanikiwa kutwa taji hilo la ligi ya mabingwa barani AFRIKA kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo.
  Pamoja na kushambulia kwa muda wote wa mchezo ZAMALEK walishindwa kupindua matokeo na goli lao pekee kwenye mchezo huo wa jana lilifungwa na STANLEY OHAWUCHI katika dakika ya  62 ya mchezo huo ambalo pia halikusaidia chochote kwao.
   Mamelodi Sundowns inakuwa timu ya pili toka AFRIKA KUSINI kutwa taji la ligi ya mabingwa barani AFRIKA baada ya ORLANDO PIRATES  kufanya hivyo  mwaka 1995 yaani miaka 21 iliyopita.

  No comments

  Post Top Ad