• Breaking News

  Kwanini Imechukua Muda Mrefu Kwa Scorpion Kukamatwa na Jeshi la Polisi?

  SCORPION NA JESHI LETU LA POLISI
  Pamoja na kwamba kijana aliyetobolewa macho kusaidiwa kujikimu maisha yake, kuna suala ambalo halipaswi kuachwa hivi. Suala hilo ni kuwajibishwa kwa polisi wa kituo cha Buguruni, kwa misingi ifuatayo:
  1. Kwanini imechukua muda mrefu kwa scorpion kukamatwa?
  2. Kijana alipata ulemavu wa macho, anasema kituo kile kilipata taarifa mapema, ni nini kilisababisha asikamatwe?
  3. Je watu wasipotoa taarifa kwenye vyombo vya habari, hawatatendewa haki?
  4. Je jeshi la polisi linafanya kazi kwa msukumo wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuliko mtu mwenyewe kutoa taarifa?
  5. Inavyosemekana, Scorpion maeneo ya Buguruni ni maarufu sana, kwa matendo yake. Kwanini jeshi la polisi liliendelea kumungalia pasi kuchukua hatua?
  Najiuliza kwa "ukichaa" wangu. Hebu IGP wawajibishe wote ambao wanaleta sifa mbovu kwa jeshi la polisi, hususani hapo Buguruni.
  Nafikiri kwa sauti.
  Mwanamtaa
  Mabuba FKM.

  No comments

  Post Top Ad