• Breaking News

  KIM KUMBURUZA MAHAKAMANI MWANDISHI HUYU

   

  Vyombo vya habari vimekuwa kipaumbele kwenye utaoaji wa habari kwa jamii, lakini kuna baadhi ya habari zinaweza kuwa na utata ambao ukasababisha madhara kwa pande zote mbili kwa mtoaji na mpokeaji.kim-kardashian

  Baada ya tukio la kuvamiwa kwa mwanamitindo Kim Kardashian akiwa mjini Paris, mmoja wa waandishi wa habari aliandika kuwa tukio lililomtokea Kim halina ukweli wowote ila ni stori za uongo zilizotengenezwa na mwanamitindo huyo ili kupata kile ambacho wabongo huita kiki.

  Kim amemfungulia mashtaka mwandishi huyo wa habari na kutaka kulipwa kwa tuhuma za kutajwa kudanganya kwenye tukio lililomtokea majuma machache yaliyopita.Kim Kardashian

  Mwanasheria wa Kim amewasilisha barua ya kesi hiyo mahakamani, hii iwe kama fundisho kwa waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli na usahihi ndani yake.

  No comments

  Post Top Ad