• Breaking News

  Jinsi ya kubadilisha Password kwenye Computer yako bila kukumbuka ile ya mwanzo

  Mara nyingi vichwa vyetu huwa bize kiasi cha kutufanya kusahau baadhi ya mambo muhimu hivyo leo nimeonelea nikuambukize ujuzi huu wa kuweza kubadili nywila (password) kwenye Laptop ama Pc zetuhivyo fuata maelekezo kwa makini ili usipoteze muda wako kwa kusoma na kuondoka matupu 

  zipo njia mbili katika kufanikisha jambo letu hili nami nitakujuza zote mbili


    NJIA YA KWANZA.
    kwa njia ya kawaida fuata hatua hizi : 1. Right click kwenye my computer na uchague sehemu iliyoandikwa "manage" Itakupeleka kwenye computer management. Unaweza kuipata hiyo kwa kubonyeza windows button+ R then ukaandika "compmgmt.msc" then ENTER 2. Tafuta sehemu iliyoandikwa "local users and groups" Then chagua users. 3.Hapo utaona users wa pc yako. Kama ni mmoja itakuwa imeandkwa administrator. Right click hiyo administrator then chagua "set password"  4.Hapo itakwambia uandike hiyo password na uconfirm (yaani pasword unayoitaka), kazi itakuwa imeisha na utaweza ku log in kwa kutumia password mpya.
  NJIA YA PILI
  Cmd ni kifupi cha neno command prompt. Hii hupatikana kwenye kila computer na hufanya kazi nyingi sana kuliko tunavyoweza kudhani.hii inauwezo hata wa kufufua flash au memory card zilizokufa. Leo tutaelezana kuhusu somo letu la leokuhusu kuchange pasword ya computer yako. Unaweza kufanya hivyo kwa kufata hatua hizi rahisi. 1. click Windows button+ R. Then andika cmd then enter. 2. Kitafunguka kipage cheusi chenye maandishi meupe. Hicho ndicho huitwa Cmd. Yaan command prompt. 3. Andika net user then ENTER itakuonesha account zote zilizopo kwenye pc yako. Mara nyingi utakuta watu wanaweka guest account na administrator account. 4. Andika met user "jina la account" then * mfano net user administrator * then ENTER. Itakuomba uweke password, andika yoyote unayoitaka (lakini haitaonekana hivyo wewe andika tu hakikisha unakumbuka unachokiandika) then ENTER. Itakuomba uconfirm password uliyoiandika confirm hiyo password then ENTER. 5. mpaka hapo Utakuwa umemaliza kubadilisha password kwenye kifaa chako yako.
  kama kuna sehemu imekuchanganya au ungependa kutoa shukrani zako niachie maoni yako hapo chini
  KIDOKEZO
  Tumia ujuzi wako kuinufaisha jamii na sio kubomoa jamii tunaelekezana kwaajili ya faida na sio kuleta hasara kwa wengine hivyo ikiwa utatumia hili kwa kufanya uharifu mimi sihusiki kwa namna yeyote ahsante kwa kutembelea blog yetu

  No comments

  Post Top Ad