• Breaking News

  Chombo kilichoenda sayari ya MARS chazua wasiwasi  Bado hakuna taarifa zozote kuhusu chombo cha anga za juu cha mataifa ya Ulaya ambacho kilikua safarini kwenda sayari ya MARS
   
  Chombo kilichoenda sayari ya MARS chazua wasiwasi
   
  Bado hakuna taarifa zozote kuhusu chombo cha anga za juu cha mataifa ya Ulaya ambacho kilikua safarini kwenda sayari ya MARS ambapo kilitarajiwa kutua kwenye sayari hiyo hapo jana.

  Hali hiyo imezua wasiwasi ambapo wataalamu wamesema mawasiliano na roboti iliyo kwenye chombo hicho cha Schiaparelli yalikatika chini ya dakika moja kabla ya wakati ambao chombo hicho kilitarajiwa kutua katika sayari hiyo.

  Setilaiti zinazoizunguka sayari ya MARS zimejaribu kufanya uchunguzi kubaini hatma ya chombo hicho kilichojaribu kutua, bila mafanikio.

  Kuna wasiwasi kwamba roboti hiyo ilianguka vibaya kwenye sayari hiyo na kuharibika.

  Chombo hicho kilikuwa na muda wa chini ya dakika sita kupunguza kasi yake ya kilomita 21,000 kwa saa kiasi cha kukiwezesha kutua salama kwenye sayari hiyo.

  No comments

  Post Top Ad